Mdau wa soka @julius_mtatiro ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru hakusita kutoa maoni yake hapo jana akiwa anafatilia Mwananchi Day ambapo gumzo mojawapo ni Haji Manara kuingia uwanjani na kutambulisha Wachezaji wakati amefungiwa kujihusisha na soka kwa miaka miwili.
DC Mtatiro ambaye ni Mfuatiliaji mkubwa wa soka alijibu kwenye comments baadhi ya Watu waliokuwa wakihoji uhalali wa Manara kuingia uwanjani na kusema kisheria hakuna kosa alilotenda Haji Manara.
“Kisheria hakuna kosa alilotenda, hapo uwanjani kumekuwa na mambo mawili, la kwanza ni sherehe ya Yanga inayosimamiwa na Yanga kama klabu“.
“Halafu kuna mechi ya kimataifa ya kirafiki kati ya Yanga na Vipers ambayo inasimamiwa na TFF, tukio alilosimamia Haji la kutambulisha Wachezaji na kusherehesha halimo kwenye masuala yanayosimamiwa na TFF, CAF au FIFA n.k ndiyo maana baada ya kusherehesha Haji ameondoka uwanjani ili kuendelea na kifungo alichopewa na TFF, nadhani sasa kisheria nimeeleweka”