Kalonzo Musyoka Asema Kulikuwa na Wizi Mkubwa wa Kura Eneo la Mlima Kenya



Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka alidai kura za Mlima Kenya ambapo ni ngome ya mgombea urais wa UDA William Ruto zilifanyiwa ukarabati fulani
Mwanachama huyo wa Azimio la Umoja One Kenya Coalition Party alidokeza kuwa hana uhakika kuhusu hesabu inayoendelea ya IEBC katika ukumbi wa Bomas of Kenya
Awali bodi ya uchaguzi ilipuuzilia mbali madai kwamba jumla ya kura 10,000 zilihesabiwa katika eneo bunge la Kiambu Mjini na kumpendelea Ruto
Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka amedai kuwa kulikuwa na wizi mkubwa katika eneo la Mlima Kenya lenye utajiri wa kura na kumpendelea mgombea urais wa United Democratic Alliance (UDA) William Ruto.

Kalonzo Musyoka Asema Kulikuwa na Wizi Mkubwa wa Kura Eneo la Mlima Kenya
Kalonzo Musyoka apiga kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2022. Picha: Kalonzo Musyoka.
Mwanachama huyo wa Azimio la Umoja One Kenya Coalition Party alisisitiza kuwa kura zilifanyiwa ukarabati katika eneo la Kati mwa Kenya, ambalo ni ngome ya Ruto.

"Tuna habari za kuaminika kuwa katika vituo vingi vya kupigia kura, mpiga kura angepewa karatasi sita hadi saba za mgombea urais pekee. Hiyo inaelezea tofauti kati ya wagombea wa ugavana, useneta na wengine.

Seneta Gideon Moi Aoshwa na Mawimbi ya William Ruto Baringo
"Katika eneo la Mlimani, unapata kwamba William Ruto aliibuka na kura milioni 1 zaidi ya magavana walivyojumlishwa. Hiyo inakuambia nini? Haya ni mambo ambayo lazima tukomeshe ikiwa tutakuza demokrasia ya nchi hii," Kalonzo aliambia TV 47.


Makamu huyo wa zamani wa rais alionyesha imani kuwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) itamtangaza mgombea urais wa Chama cha Muungano wa Kenya Raila Odinga kuwa mshindi.

Awali IEBC ilipuuzilia mbali madai kwamba jumla ya kura 10,000 zilihesabiwa katika eneo bunge la Kiambu Mjini na kumpendelea Ruto.

Ilikuwa imeripotiwa kuwa matokeo ya urais katika fomu 34B ya eneo bunge hilo yalionyesha kuwa Ruto alipata kura 51,050 dhidi ya 14,860 za Raila Odinga.

Hata hivyo, bodi ya usimamizi wa uchaguzi ilibaini hitilafu hiyo na kurekebisha takwimu kosa hilo ikibaini kuwa DP alipata kura 41,050.

Alinur Mohammed Azua Hisia Mseto Baada ya Ujumbe wa The 5th
Jumamosi, Agosti 13 asubuhi, TUKO.co.ke iliripoti kuwa mgombea mwenza wa Raila Martha Karua alielezea imani yake kwamba muungano huo utashinda urais wa 2022.

Akiwahutubia viongozi waliochaguliwa na Azimio mnamo Jumamosi, Agosti 13, katika Ukumbi wa Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC), Karua alidai kuwa walikuwa wameshinda kinyang'anyiro cha kuelekea Ikulu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad