No title



 
Kaoneka: Mandonga fanya mazoezi
BONDIA Shaban Kaoneka amempa neno bondia mwenzake Karim Mandonga kuwa kama anataka kufanya vizuri katika mchezo huo hana budi kufanya mazoezi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, bondia huyo alisema ngumi ni mchezo unaohitaji vitendo zaidi kuliko maneno na kumhimiza mwenzake huyo kujipanga kwa kufanya mazoezi kama atahitaji warudiane.

Kaoneka ndiye aliyempiga Mandonga katika pambano la utangulizi la kumsindikiza Seleman Kidunda dhidi ya Erick Katompa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), mwishoni mwa wiki iliyopita Songea mkoani Ruvuma.

Mandonga alipigwa raundi ya nne na pambano hilo kukatishwa kuokoa maisha ya bondia huyo wa Morogoro.


 
“Mandonga akitulia anaweza kuwa bondia mzuri, aache maneno mengi afanye mazoezi kwa sababu mashabiki watakupenda unavyoongea sasa lakini baadaye watakuchoka ikiwa utaendelea kupoteza,” alisema.

Alisema wakati huu, bondia huyo anahitaji kutafuta mwalimu mzuri atulie ikiwezekana miezi miwili kujiweka imara ili kurudi tofauti na kiushindani.

Kaoneka alisema Mandonga anataka warudiane na kwamba yeye yuko tayari ila anamshauri kabla ya kukutana tena anapaswa kurudi katika ushindani mzuri ili pambano lipate kuvutia.


Kabla ya pambano hilo, Mandonga alitamba na kumtisha mpinzani wake kuwa ajipange kwani hatotoka salama kiasi cha kuwaaminisha mashabiki wa ngumi kuwa huenda angeshinda lakini mambo yalimwendea tofauti.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad