Familia ya Jaramogi Oginga Odinga kutoka eneo la Bondo imeelekeza macho yake kwa kiti cha urais, ikitumai kuwa Raila Odinga ataapishwa kuwa Rais wa Kenya baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo na Mwenyekiti wa IEBC.
Endapo mgombea huyo wa urais wa Azimio la Umoja One Kenya atashinda, atakuwa ametimiza moja ya ndoto zake baada ya majaribio manne kufeli kwani Kiongozi huyo na familia yake wamepitia nyadhifa nyingi isipokuwa kiti cha Urais.
Jaramogi Oginga Odinga, alikuwa makamu wa kwanza wa rais wa Kenya, huku Odinga mwenyewe akiwahi kuwa Waziri Mkuu wakati wa enzi ya Kibaki na kakake mkubwa Dkt. Oburu Oginga aliwakilisha Kenya katika Bunge la Afrika Mashariki.
Kenya: Mwenyekiti IEBC atishia kuwatimua Mawakala
Kiongozi wa ODM, Raila Odinga (wa pili kushoto) Katika picha na nduguze, Oburu Oginga (kushoto), Dkt. Wenwa Akinyi na Ruth Adhiambo mjini Kisumu, Kenya.
Kenya: Mwingine akamatwa kwa upotevu wa masanduku ya kura
Wanafamilia wengine wa Odinga, wamewahi kushikilia nyadhifa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na dadake Odinga Akinyi Wenwa, ambaye aliwakilisha Taifa la Kenya katika nchi tofauti huku katika uchaguzi huu, wanafamilia watatu wa Odinga wakinyakua viti viwili huko Siaya na Kisumu.
Awali, Dkt. Oginga aliwahi kutangazwa kuwa seneta mpya wa Siaya, huku dadake mdogo Ruth Odinga akishinda kiti cha mwakilishi wa wanawake Kisumu ambapo Dkt. Oginga alipata kura 285,595, akimshinda mshindani wake wa karibu, Okinda Julius Okongo, aliyesimamia 33,898.
Akiongea mara baada ya ushindi, Dkt. Oginga lisema ushindi huo kuwa moja ya hafla kubwa kwake kutokana na umri wake na watu aliokuwa akishindana nao.
Kenya: Matayarisho makabidhiano Ofisi ya Rais yaanza
Jaramogi Oginga Odinga
Kenya: Waangalizi wa uchaguzi wadai kutengwa
Suala la umri lilitawala kampeni hizo, huku wengi wakisema kuwa akiwa na umri wa miaka 78, Dkt. Oginga alifaa kuwapa nafasi viongozi wachanga, lakini akasisitiza kuwa Bunge la Seneti ni kundi la wanasiasa wazoefu na wazoefu.
Bado tunasubiri matokeo ya kiti cha Urais nchini Kenya ili kufahamu kama ni Raila Odinga ama ni William Ruto, tuwe na subira.