Kimenuka..Haji Manara na Rais wa Yanga Hersi Said Wafunguliwa Mashtaka na TFF Kisa Yanga Day


Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungulia mashtaka ya kimaadili Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said na aliyekuwa Ofisa wa Klabu hiyo Haji Manara “Kamati ya Maadili ilimfungia miaka miwili Manara kujihusisha na shughuli yoyote ya mpira wa miguu lakini ameshindwa kutekeleza adhabu hiyo”


Kamati imesema Hersi amefunguliwa mashtaka kwa kwenda kinyume na ibara ya 16(1) (a) ya Katiba ya TFF pamoja na ibara ya 1(6) ya Katiba ya Yanga.

Taarifa ya TFF inasomeka ———> “Baada ya Manara kuadhibiwa na Kamati ya Maadili ya TFF, Sekretarieti ilimwandikia barua Mhandisi Said kuhakikisha Klabu yake inaheshimu uamuzi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili tayari amepelekewa mashtaka hayo, walalamikiwa watapewa mashtaka na mwito mara baada ya Kamati kupanga tarehe ya kusikiliza mashtaka hayo”.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad