Moshi. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne tayari wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kusikiliza kesi inayowakabili.
Sabaya na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumatatu Agosti 29, 2022 ambapo wanakabiliwa na mashitaka saba likiwamo kosa la uhujumu uchumi, kuongoza genge la uhalifu pamoja na kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Juni Mosi mwaka huu, Sabaya na wenzake wanne wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kusomewa mashtaka yanayowakabili mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey.