Kipa Azam ageuka lulu Ulaya



 
AZAM FC ipo kambini Misri ikijifua kwa msimu ujao wa mashindano ya ndani na yale ya kimataifa, lakini kipa wao zamani, Razack Abalora (25) ameendelea kutamba Ulaya akiwa na timu ya Sheriff Tiraspol ya Moldova kwa sasa.

Azam FC iliachana na Abalora mwaka 2020 baada ya kumtumia kwa miaka miwili Januari mwaka huu kipa huyo alijiunga na mabingwa Ligi Kuu ya Moldova na kuweka rekodi ya kipekee katika Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopo hatua ya mchujo kwa sasa.

Rekodi hiyo ni ya kucheza michezo minne mfululizo katika mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya klabu Ulaya bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa.

Ushindi wa bao 1-0 ambao Sheriff Tiraspol iliupata dhidi ya Maribor ya Slovenia uliifanya itinge raundi ya tatu ya mashindano ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini ukamfanya Abalora atimize dakika 360 bila kufungwa bao katika mashindano hayo.

Mchezo wa kwanza wa Abalora ulikuwa ni dhidi ya Znjriski kwenye raundi ya kwanza timu hiyo ikicheza ugenini na kutoka suluhu kisha kushinda nyumbani kwa bao 1-0 kabla ya kupangwa kuvaana na Maribor na ugenini ikatoka nayo suluhu kisha juzi kati ikashinda tena 1-0. Ushindi huo umeifanya timu hiyo itingine raundi ya tatu na sasa itakutana na Viktoria Plzen ya Czech.

Baada ya kuachwa na Azam, Abarola alitimkia Asante Kotoko ya Ghana kisha akatua Sheriff Tiraspol. Timu hiyo ndio aliyokuwa akiichezea winga wa Simba, Peter Banda.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad