Kocha Mosimane Aukubali MZIKI wa Young Afrians...Kunogesha Siku ya Wananchi



Aliyekua Kocha Mabingwa wa zamani Barani Afrika Klabu ya Al Ahly ya Misri ‘Pitso Mosimane’ ameupongeza Uongozi wa Young Africans kwa kumualika Tanzania na kuwa sehemu ya Shamra Shamra za Wiki ya Mwananchi.


Young Africans Kesho Jumamosi (Agosti 06), itahitimisha Wiki ya Mwananchi kwa kufanya Tamasha ya Siku ya Wananchi, Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku kikosi chake kikitarajiwa kucheza mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Uganda, Vipers SC.


Mosimame ametoa Shukurani kwa Uongozi wa Klabu hiyo Kongwe katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari Viwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam.


Amesema alikua na Shauku ya kutaka kushiriki katika Wiki ya Mwananchi, baada ya kuifuatilia Young Africans kwa muda mrefu kupitia vyanzo vyake vya Habari, hivyo hana budi kuushukuru Uongozi kwa kumualika.


Mosimame pia amelipongeza Benchi la Ufundi na Young Africans pamoja na Wachezaji kwa kufanya kazi nzuri msimu uliopita ‘2021/22’ na kutwaa Mataji matatu.


“Nimekuwa na shauku ya kuona na kushiriki katika Wiki Ya Wananchi na napenda kuwapongeza Young Africans SC na Rais Hersi Said kwa kushiriki matukio ya kijamii na kuinua soka la vijana.”


“Pia nipende pia kumpongeza Kocha na Benchi lake la ufundi kwa kushinda Makombe Matatu na mimi pia ni mshindi wa Makombe Matatu mara Tatu”


“Niliona hamasa kubwa ya mpira kwenye Sherehe za Ubingwa (parade) kwa Mashabiki wa Klabu hii pendwa na hamasa hii ilipelekea Dunia nzima kuangalia kile walichofanya Yanga kwenye mapokezi ya Ubingwa na ilinivutia kupita kiasi” amesema Mosimane

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad