Pitso Mosimane yupo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria tamansha la Siku ya Wananchi linalofanyika Agosti 6 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
KOCHA za zamani wa Al Ahly, Pitso Mosimane amekuwa kivutio, jioni leo kwenye mazoezi ya mwisho ya Yanga kwenye uwanja wa Mkapa kabla ya kumvaa bingwa wa Uganda hapo kesho, Jumamosi kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi.
Pitso ambaye anatajwa kuwa mmoja wa makocha bora Afrika kwa sasa, alionekana kuwa mwingi wa tabasamu usoni mwaka huku akizunguka na kuteta mawili matatu na wenyeji wake.
Mtaalamu huyo muda mwingi alionekana na Sadi Kawemba ambaye ni Mkurugenzi mpya wa mashindano wa Yanga.
Miongoni mwa watu ambao Pitso alipata nafasi ya kuteta nao ni pamoja na makocha wa Yanga na Vipers, Nasreddine Nabi na Roberto Oliveira maarufu kama Robertinho.
Wakati huo, Vaipers ilikuwa imemaliza programu zao za mazoezi huku Yanga ikiingia kujiweka sawa, Khalid Aucho alitumia mwanya huo kusalimiana na ndugu zake hao wa Kiganda.
Mara baada ya mazoezi kuanza Pitso alikuwa makini kifuatilia programu za mazoezi ya Nabi huku akipiga stori za hapa na pale na viongozi mbalimbali wa Yanga, akiwemo rais, Injinia Hersi Said.
Pitso anashikilia rekodi ya kutwa Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na timu mbili tofauti ambazo ni Mamelod ya nchini kwao Afrika Kusini na Al Ahly ambayo ameachana nayo wiki chache zilizopita.