Mtangazaji mwenye utata mwingi kutoka nchi Jirani ya Uganda kwa jina Lucy Mbabazi amewachekesha Wakenya kwa mara nyingine tena baada ya kupakia video akidai kwamba anafuatilia shughuli nzima ya kuhesabiwa kwa kura za urais nchini Kenya mubashara kweney runinga.
Katika video hiyo ambayo aliipakia kwenye ukurasa wake wa Facebook, Mbabazi aliifuatisha kwa maneno kwamba anafuatilia kuhesabiwa kwa kura hizo huku akionekana mwenye kuhaha sana pasi na kutulia kaam mtu anayesokotwa na tumbo.
Alidokeza kwamba shinikizo la kufuatilia mchakato huo kama unavyoendelea kutoka kituo kikuu cha kuhesabu kwa kura Bomas Nairobi na shinikizo hilo tayari limeshamzushia kuendesha tumbo.
“Mimi ninapofuatilia kuhesabu kura za Wakenya na shinikizo nililo nalo ni kweli kana kwamba ni Mkenya. Nadhani hata nimepata ugonjwa wa Kuhara,” Mbabazi aliandika kwenye video hiyo.
Mashabiki wake walizua utani mkubwa kwenye ukurasa huo wake huku wengine wakimuambia kwamba anapenda kufuatilia mambo ya Kenya kwa sababu damu yake ipo huku.
Itakumbukwa hii si mara ya kwanza kwa mtangazaji huyo kuzua mjadala mkali nchini haswa wakati wa mashindano ya riadha huwa anasema baadhi ya wanariadha wa Kenya wana mizizi ya ukoo wao nchini Uganda.
“Una presha kwa sababu unawapenda sana wakenya. Huwa ninaona muda mwingi unapenda kuwazungumzia sana. Wewe mwanamke lazima uwe na damu ya Kenya,” shabiki mmoja alimwambia.
Bila shaka shughuli ya kuhesabu kura kwa amani na haki nchini Kenya ni jambo geni kwa Waganda wengi ambao wamezoea udhalimu wa rais wa muda wote Yoweri Museveni ambapo mara nyingi uchaguzi unapofanywa huwa si wa haki kwa asilimia kubwa kama mataifa mengi yenye ukomavu kidemokrasia.