Kutana na Mke Halali wa Producer P Funk Majani....Sio Kajala Masanja


Kushoto ni mke halali wa Majani. Anaitwa Hidaya, ameolewa rasmi na Majani mwaka 2014 ila uhusiano wao wa kimapenzi ulianza miaka minne nyuma kabla ya ndoa (2010)

Majani na Hidaya wamefanikiwa kupata watoto watatu. Mwaka 2015 na mwaka 2018 zilikuwa zikizuka skendo kwamba Kajala amerudiana na Majani, Skendo hizi zilikuwa zikiathiri sana ndoa ya Majani na Hidaya lakini hazikuwahi kusababisha ndoa hiyo Kuvunjika kwani ukweli ulikuwa unakuja kujulikana, kwamba Majani na Kajala hawajarudiana.

Ikumbukwe kwamba Majani na Kajala waliachana zamani sana, enzi hizo Paula akiwa mdogo sana. Kajala anadai kwamba kilichofanya waachane ni suala la Kipigo, alikuwa anachezea sana kipigo kutoka kwa Majani.

Baada ya Kajala kuachana na Majani alikurupuka akaenda kuolewa na mtu asiyemfahamu sana na bahati mbaya tabia za huyo mme wake hazikuwa nzuri sana, hivyo zikamuingiza mkengeni Kajala na akafungwa Jela na Mme wake baada ya wote kukutwa na hatia ya kuuza nyumba ambayo awali Takukuru walizuia isiuzwe.

By Sajomedia

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad