Lori laziba barabara mamia wakwama Morogoro



Morogoro. Mamia ya wasafiri na magari yanayotumia barabara ya Morogoro - Dar es Salaam wamekwama kwa zaidi ya saa sita baada ya lori lenye shehena ya magogo kushindwa kupanda mlima na kufunga barabara eneo la Mikese na kusababisha foleni.

Akizungumza na Mwananchi Digital akiwa kwenye eneo la tukio leo Jumamosi Agosti 13,2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim amesema lori hilo lilifunga barabara usiku wa kuamkia leo.

Amesema jitihada zinazofanywa kwa sasa ni kupata mashine itakayoweza kunyanyua magogo na kusogeza gari kando ya barabara.

"Mimi mwenyewe nipo hapa eneo la tukio tunachofanya kwa sasa ni kuruhusu magari kupita kwa awamu kwenye haka kamwanya kadogo angalau kupunguza foleni, maana foleni ni ndefu na hata hivyo magari yanatembea kidogokidogo," amesema Muslimu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad