Mabondia Karim Mandonga Amjibu Shaban Kaoneka Baada ya Kulalamika Kutohojiwa na Vyombo vya Habari Licha ya Kushinda


Mabondia Karim Mandonga na Shaban Kaoneka wamerudi tena kwenye headsline kufuatia kauli ya Bondia Shaban Kaoneka aliyoitoa siku ya jana akizungumza na Wasafi Media ndani ya dimba la Benjamin Mkapa alipokwenda kushuhudia Tamasha la Simba Day.


Kwenye mahojiano hayo Kaoneka alisema, "Mandonga amepata bahati kuliko mimi, waandishi wa habari wakati mwingine naona kama mnakuwa wanafiki, hamjaniita hata ofisini kwenu kunihoji, mbona Mandonga mnamfanyia surprise nyingi, mimi niliyeshinda nakuwa masikini, aliyepigwa anakuwa tajiri,” alieleza Shabani Kaoneka akiiambia Wasafi Media.


Kauli hiyo imemuibua Karim Mandonga Mtu Kazi ambaye hivi karibuni amelamba madili mbalimbali, yeye ameeleza kuwa, hata yeye hajawahi kuwaza kama kuna siku atasimama kama mtu maarufu mkubwa hivyo Kaoneka hapaswi kumlaumu mtu yoyote yule. Ajifunze kumshukuru Mungu kwa kila jambo.


"Dah Shabani ndugu yangu me naamini kabisa ridhiki inatoka kwa mafungu na kwa muda maalumu alieupanga Mungu suala la nani afanikiwe nani aishie njiani ni majukumu ya Allah mimi na wewe hatupaswi kumlaumu mtu yoyote yule.


"Katika tasnia hii ya mchezo wa ngumi na watu wa media kiujumla hata mimi sijawahi kuwaza kwamba ipo siku nitasimama kama SUPERSTAR MKUBWA but all in all tujfunze kumshukuru Mungu kwa kila jambo. KAMA IPO IPO TU" ameandika Bondia Karim Mandonga.


Una mtazamo gani juu ya hili...


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad