Mahakama yaamuru dereva wa Mabasi aliyetrend alipwe Milioni 150, ‘Mdaiwa alitumia picha yake



Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imeiamuru Kampuni ya Bima ya Dexter Insurance kumlipa Dereva wa Kampuni ya New Force, Waubani Linyama maarufu kama ‘Ndugu Abiria’ fidia ya Tsh. 150 milioni kwa kosa la kutumia picha yake kwenye mitandao ya kijamii kufanyia biashara na kijipatia faida.

Itakumbukwa Mwezi July mwaka jana Ayo TV na millardayo.com zilifanya mahojiano maalumu na Linyama, Dereva ambaye Memes zake zilitrend mitandaoni ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuna Kampuni imetumia picha yake na anaidai Mil. 200”

Mahakama ya Kinondoni pia imetoa zuio la kudumu dhidi ya kampuni ya udalali ya Dexter Insuarance kutoendelea kutumia picha ya Linyama kwenye matangazo yao ya biashara, Linyama akiwakilishwa na Wakili wake, Ferdinand Makore ambaye alifungua kesi katika Mahakama hiyo akiomba Kampuni hiyo ya bima imlipe fidia ya Tsh. Milioni 200 kwa kuituma picha ya Mdai huyo kwenye mitandao ya kijamii kwa lengo la kujipatia faida au biashara

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad