Majeshi Wachukua Usukani Nyumbani Kwake William Ruto Sugoi




Majeshi Wachukua Usukani Nyumbani Kwake William Ruto Sugoi
Rais mteule William Ruto. Picha: William Ruto.
Nyumba na mali zingine zake naibu rais sasa zinalindwa na kitengo cha CIPU cha Polisi wa Utawala.

Baada ya maafisa wa GSU kuchukua jukumu la kusimamia makazi hayo, walianza kukagua kila gari lililokuwa likiingia na kutoka nyumbani humo.

Museveni, Buhari Wampa Pongezi Ruto kwa Kutangazwa Rais Mteule
Wenyeji wa Sugoi walikuwa wamejitokeza kwa wingi kusherehekea ushindi wa Ruto, lakini walikataliwa na maafisa hao kuingia.


Mnamo Jumatatu, Agosti 15, mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Wafula Chebukati alimtangaza Ruto kuwa rais aliyechaguliwa kihalali.

Ruto alipata kura 7,176,141 ambazo ni asilimia 50.49% ya kura zote zilizopigwa; aliafiki matakwa ya katiba ya 50% pamoja na kura moja ili kutangazwa kuwa rais.

Ruto pia alipata asilimia 25 ya kura zote katika kaunti 39.


Katiba inadai mgombea aliyeshinda apate 25% ya kura katika angalau nusu ya jumla ya idadi ya kaunti.

Hasimu wake wa kisiasa na mgombea urais wa Azimio la Umoja One Kenya Coalition Party Raila Odinga aliibuka wa pili kwa kura 6,942,930 (48.85%).

Wagombea hao wawili wa urais wakati wa kuhesabiwa kwa kura walikuwa wamekabana koo huku wasiwasi ukiendelea kuwagubika wananchi.

Magazetini Agosti 16: William Ruto Alizungumza na Raila Kabla ya Kutangazwa Rais Mteule
Ni hadi Agosti 15 ambapo Wakenya walipata mshindi wa wazi wa kinyang'anyiro cha urais cha Agosti 9 baada ya siku nyingi za matarajio na wasiwasi.


Akizungumza wakati akitangaza mshindi, Chebukati alisema:

"Mimi Wafula Chebukati, mwenyekiti wa IEBC ninatangaza kwamba Ruto William Samoei wa kitambulisho Namba 6847208 amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa mujibu wa kifungu cha 138."

Katika hotuba yake ya kukubali ushindi huo, Ruto aliahidi kufanya kazi na viongozi wote ili kusiwepo na yeyote ambaye anayehisi kutengwa katika uendeshaji wa nchi.

Rais mteule alimpongeza mpinzani wake mkuu Raila Odinga kwa ushindani mkali.


"Ninataka kumshukuru mshindani wangu Raila Odinga kwa kampeni ambayo sote tuliangazia masuala ambayo tuliuza ajenda kwa watu wa Kenya," Ruto alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad