Makarani Sensa Hatarini Kufungwa Miezi Sita




SERIKALI imeonya makarani wa sensa ya watu na makazi waache kupiga picha na wananchi wanapoifanya kazi hiyo.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk Albina Chuwa alisema ni kosa la jinai kwa makarani wa sensa kupiga picha wakiwa katika kaya za watu na kuzitumia katika mitandao ya kijamii.

Dk Chuwa alitoa onyo hilo alipozungumza na waandishi wa habari wakati akikagua maendeleo ya shughuli hiyo mkoani Iringa.

“Kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu sura ya 351 ni kosa kumrekodi video au kumpiga picha mwananchi ambaye unamuhoji ili kupata taarifa zake… kwenda kwenye kaya ya Mtanzania mwenzako na kurekodi mambo yaliyopo kwenye kaya yake yawe mazuri au mabaya haikubaliki na kinyume na sheria,” alisema.


Dk Chuwa alisema adhabu ya kufanya hivyo ni kifungo cha miezi sita jela au faini ya Sh milioni mbili au vyote kwa pamoja.

Akizungumzia maendeleo ya shughuli hiyo nchini kote, Dk Chuwa alisema serikali inaridhishwa na mwenendo wa sensa na kwamba wanatarajia itafanikiwa kwa kiwango kinachokusudiwa.

“Wananchi wa Iringa mkiniona katika maeneo yenu mjue nimefika kuangalia maendeleo ya ufanyaji wa kazi za makarani wetu, naomba mnipe ushirikiano pale nitakapohitaji kujua chochote kutoka kwenue” alisema Dk Chuwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad