HAJI Manara msemaji wa Yanga anayetumikia kifungo cha kukaa nje miaka miwili, alichoadhibiwa na kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ametoa ufafanuzi wa kwa nini ametambulisha wachezaji wa timu hiyo.
Manara baada ya kumaliza kazi ya kutambulisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi, amesema kazi hiyo kama MC mwalikwa na ahusiki na mambo ya soka kabisa.
Adhabu ya Manara aliyopewa na kamati ya nidhamu ya TFF, inamtaka asijihusishe na kitu chochote kinachohusiana na michezo.
Manara amesema "Nipo hapa kama walivyoalikwa kina Zembwela, Dakota na Maulid Kitenge, nimemaliza kazi yangu naondoka kabisa uwanjani kwenda kwenye kazi ya UMC Kidogo."
Alidakia Kitenge aliyesema "Tena ni MC tuliyemtoa Manzese mtaani, hivyo ahusiani na mambo ya soka."
Manara ni kama ametoa ufafanuzi kwa mashabiki waliyokuwa wakijiuliza kwa inakuaje Manara anatambulisha wachezaji wakati ana adhabu.