Jamani huyu kaka yangu nini kimempata siku hizi? Mbona misamaha mingi? Alafu mama hayuko Sawa maskini. Niko busy na connection na umbea mpaka sijafatilia Issue yake.
Mi simpendagi Haji siku hizi, toka aniharibikie kiki siku ya harusi yake. Yani aliweka bonge la ulinzi kwenye harusi yake, hakuna mtu kupiga picha kasoro mpiga picha wake. Ila mimi nikapambana mpaka nikapata picha, ile nimeposti tu insta kuwaambia watu waje kwenye app kuona harusi yake eti na yeye akaachia professional photos akawasambazia na mastaa Dm na WhatsApp waposti. Dah, nililia machozi, Yani hakujali dadake nimetumia pesa ngapi kupata zile picha. Hivi angeniacha nikatamba nazo kwa siku moja tu au mbili nirudishe pesa yangu, then akaachia zake angepungukiwa nini? Roho mbaya tu. Simpendi toka siku ile maana ni kama nilipoteza pesa kulipia zile picha…Hakuna event nilipata hasara kama ile.
Ila hata kama simpendi wamsamehe bwana. Huyu kaka kapambana sana kufika hapo. Haji katokea life gumu, kapigana mnooooo kufika hapo. Wamwangalie kwa jicho la huruma aiseee. Hakuna asie mkosefu duniani. Cha msingi kajishusha na kaomba msamaha……
This is not about Haji, it’s about soccer la Tanzania as a whole, inabidi wizara ya michezo na yenyewe I recognize kuwa bila haji Manara soka ilishakufa Tz. Wao kama wizara na hiyo TFF wote walishindwa kuipa kiki soccer Haji pekee ndo alieweza kuitrendisha soccrt ya TZ. Soccer Ilibaki kushabikiwa huko ushahili tu, ila Haji kairudisha soka nchi nzima. Hapana kwa kweli inabidi mchango wake utumike kama kigezo cha kumsamehe…. Na je wamefikiria effects za kumkalisha kando kwa miaka 2? Wanadhani wanamkomoa Haji pekee? Wanalikomoa na soka la nchi. @wizarayamichezo embu tumieni busara basi, acheni mihemko…