Mashabiki "Mke wa NEYO Anatafuta Kiki Kumtuhumu Mumewe Kutembea na Makahaba


Baada ya kashfa nzito inayomkabili Ne-yo, iliyovujishwaa na mkewe bibie Crystal Smith mwishoni mwa wikiendi kuhusu mwanamuziki huyo kujihusisha na vitendo vya usaliti, kwa kutoka kimapenzi na wanawake wenye kufanya biashara ya kuuza miili yao (Machangudoa), na kisha Crystal kuweka wazi maamuzi yake kuwa sio mke tena wa Ne-yo, mapya yaibuka!


Kwenye moja ya video siku jana ambayo Crystal aliiposti kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa ndani ya gari yake anasikiliza muziki, mashabiki wakagundua kwenye kidole chake kuna pete ya ndoa jambo ambalo mashabiki wamelitafsiri kuwa madai ya kuachana sio ya kweli kwani alikuwa anatafuta kuzungumziwa.


Aidha, komenti za kumponda zilikuwa ni nyingi zikimshutumu kwamba anatafuta kuongelewa, nae Crystal hakubaki nyuma aliweza kuzijibu chache akisema kwamba kuachana na Ne-yo hakumzuii yeye kuvaa pete hiyo ambayo ameitaja kuwa ni ya gharama kubwa iliyonakshiwa na madini ya Almasi.


Sanjali na hilo, Ne-yo na Crystal Smith, katika ndoa yao wamefanikiwa kupata watoto watatu, ambao ni Shaffer (6), Roman (3) na Isabella mwenye umri wa miezi 13.


Je ni kiki au ni kweli wamebwagana! Unaamini lipi.. Dondosha komenti yako


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad