Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Maswali yaibuka kuhusu ushahidi wa udukuzi wa uchaguzi Kenya





Ushahidi kutoka kwa mwanaharakati wa kupinga ufisadi nchini Kenya, John Githongo, kuunga mkono madai mgombea urais, Raila Odinga, kwamba mfumo wa matokeo ya uchaguzi ulidukuliwa ili kumpokonya ushindi unashabihiana na waraka uliowasilishwa mwaka wa 2017.

Miaka mitano iliyopita, Bw Odinga pia alipinga matokeo ya uchaguzi na Mahakama ya Juu ikaamuru urudiwe.

Kurasa nyingi za waraka wa 2017 zinazoonyesha kumbukumbu - neno la kiufundi kwa rekodi ya shughuli kwenye mfumo wa kompyuta - zinaonekana sawa na zile zilizo kwenye hati ya sasa, wakati mwingine na tarehe tu zimebadilishwa.

Picha za skrini katika hati ya kiapo iliyowasilishwa na Bw Githongo na kuripotiwa kuwa kutoka kwa mtoa taarifa hata mwaka wa 2017 kuonekana miongoni mwa tarehe zilizokusudiwa kuwa za Agosti mwaka huu.


Pia kuna makosa ambayo yanaonekana kuwa rahisi kwa mfano, muda uliotolewa kama 16:54:30 jioni katika hati ya 2017 unaonekana kama 6:54:30 jioni katika wasilisho lililotolewa wiki hii, ambayo inaonekana kukosa tarakimu ya kwanza.

BBC Reality Check imegundua kwamba hati iliyochapishwa mwaka wa 2017 ilitoka kwa Makau Mutua, ambaye kwa sasa ni msemaji wa kampeni ya Bw Odinga

BBC imewasiliana na afisi ya Bw Odinga ili kuomba ufafanuzi.


Anapinga matokeo ya kumtangaza Naibu Rais William Ruto kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad