Mawakili wabishana Mdee wenzake kuhojiwa, uamuzi Septemba 2





Wakili wa Chadema, wakiongozwa na Peter Kibatala (katikati) wakiwa mahakamani
MAWAKILI wa upande wa waleta maombi wamepinga upande wa washtakiwa (Chadema), kuwahoji Halima Mdee na wenzake saba ambao waliitwa mahakamani leo kwaajili ya kuhojiwa. Anaripoti Faki Sosi na Apaikunda Mosha, Dar es Salaam … (endelea).

Mawakili hao wameweka pingamizi hilo leo Ijumaa tarehe, 26 Agosti, 2022, katika Mahakama Kuu mbele ya Jaji Cyprian Mkeha, ambapo shauri hilo liliitwa kwaajili ya kuanza kusikilizwa ambapo Mdee na wenzake wanapinga kufukuzwa uanachama wa Chadema kwa madai kuwa utaratibu ilikiukwa.

Mawakili hao wamepinga mahakama kuruhusu wateja wao kuhojiwa kwa kuwa wao ndio wanaoshitaki na kwamba upande unaotaka kuwahoji ni wa washitakiwa (Chadema).

Wakili wa washitakiwa, Peter Kibatala ameiomba Mahakama iwakumbushe amri ambazo mahakama ilitoa na Jaji Mkeha amezisoma amri hizo ikiwa ni pamoja na kuwasilishwa kwa kiapo kinzani tarehe 5 Agosti, 2022 na Mdee na wenzake kufika mahakamani tarehe 26, Agosti, 2022 saa tatu asubuhi kwaajili ya kuhojiwa.



Halima Mdee na wenzake sita wakiwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam
Wakili Kibatala amesema msingi wa hoja iliyotolewa ni dhaifu “mno” kisheria hazijaoana na maombi ya waleta maombi.

“Mahakama ikishatoa amri mikono ya mahakama imefungwa, wenzetu wameshathibitisha walioitwa na mahakama wapo, mahakama itekeleze amri yake,” amesema Kibatala.

Edson Kilatu wakili wa kina Mdee amedai kuwa pingamizi la awali linaweza kuwasilishwa na upande wowote katika shauri, “sio kama anavyodai Wakili Peter Kibatala kuwa ni silaha ya wajibu maombi.”


Jaji Mkeha amesema kuwa atatoa uamuzi tarehe 2 Septemba 2022 saa nane na nusu mchana na kuwataka Mdee na wenzake saba waliotakiwa kuhojiwa leo wasiende mahakamani mpaka mahakama hiyo itakapotoa uamuzi wa pingamizi hilo.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad