Mbosso afunguka kuzaa na mke wa Abdukiba, adai hakuwa anajua




Staa wa bongo fleva, Mbosso amethibitisha kuzaa mtoto wa kike na aliyekuwa mke wa msanii Abdukiba huku akidai kwamba hakuwa akijua kuwa mwanamke huyo aliolewa na Abdu Kiba hadi alipoambiwa na ndugu wa Diamond

Harusi ya Abdu Kiba na mwanamke husika iliteka vyombo vya habari kipindi kile, na pia inadaiwa mwanzoni Mbosso na Abdukiba waliwahi kuwa marafiki kabla hajahamia Wasafi na hata kabla Abdukiba hajamuoa huyo mwanamke na ndoa kusambaratika.


 
Akizungumza kweney kipindi cha Big Sunday kwenye runinga ya Wasafi, Mbosso alisema kwamba ni kweli tukio la kupata mtoto na aliyekuwa mke halali wa Abdukiba lilitokea lakini akasisitiza kwamba ni makosa ya kina dada ambao muda mwingi huwa hawasemi kama wapo katika mahusiano pindi wanapotongozwa.

Mbosso alisisitiza kwamba hamna uhasama baina yake ya Abdukiba na kumtaja kuwa mwanake wa ubavuni kabisa.

“Kibinadamu, katika kuzunguka tulikutana sehemu, sikuwa nafahamu kabisa kwamba aliwahi kuwa mke wa Abdukiba, naapa kabisa sikuwa najua. Siku moja nilikuwa katika mazingira fulani halafu nikaweka oda ya biriyani na sikua najua ni kutoka kwake. Ikawa sasa kama mchezo kila Ijumaa naitisha biryani na sijui kama ni mke wa Abdukiba. Aliniambia ni shabiki wangu na ikawa kawaida sasa ya biryani na ndio hivo mahusiano yakaanza na kukolea na ndio hivo kama mlivyosikia tulipata mtoto,” Mbosso alimwaga mtama.


Alisema kwamba mwanamke huyo mpaka alimfuata Kwenda tamasha tamasha alikokuwa akiburudisha Zanzibar na waliporudi Dar es Salaam wakawa wanawasiliana kwa ukaribu na mwisho wa siku matunda yakawa ni kuzaliwa kwa mtoto wa kike baina yao.

Alisema kwamba katu hakuwa anajua na kadri mahusiano yalipokuwa yanakolea ndio ndogo wake Diamond kwa jina Idd Santos alimchanua kwa kumwambia kwamba yule mwanadada alikuwa mke wa msanii na rafiki yake wa karibu, Abdukiba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad