Mchezaji Molinga ni Zanaco tena




KLABU ya Zanaco kutoka nchini Zambia iko kwenye mazungumzo na aliyekuwa mshambuliaji wa Namungo na Yanga, David Molinga ‘Falcao’.

Hatua hiyo inajiri baada ya Molinga kushindwa kuongezewa mkataba mpya na Namungo hivyo kuachwa akiwa mchezaji huru hali inayowavutia mabosi wa Zanaco kuhitaji saini yake.

Chanzo kutoka ndani ya klabu ya Zanaco kilieleza, Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Kelvin Kaindu alifanya mazungumzo ya moja kwa moja na Kocha wa Namungo, Hanour Janza akiulizia ni kwa jinsi gani anaweza kumpata staa huyo ili kwenda kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji.

Molinga alishindwa kuongezewa mkataba mpya huku sababu kubwa ikielezwa ni kushuka kiwango hali iliyomfanya kocha, Janza kwenda kwao Zambia na kurejea na mshambuliaji, Alidor Kayembe aliyesajiliwa msimu huu akitokea kwa mabingwa wa nchi hiyo Red Arrows.

Mwanaspoti linatambua Molinga alianza kuwasiliana na Kaindu wakati kikosi cha Zanaco kilipokuja nchini kucheza mchezo wake wa kirafiki na Singida Big Stars Agosti 4.

Kama dili hilo litakamilika hii itakuwa ni mara yake ya pili kwa nyota huyo kurejea Zambia baada ya kuichezea Zesco United kabla ya kutua Namungo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad