Mchezaji wa Sierra Leon akosa kuhudhuria harusi yake na kwenda Sweden kusaini mkataba na klabu mpya kisha kumuomba ndugu yake amuwakilishe katika harusi hiyo
Mohamed Buya Turay akihojiwa na gazeti la nchini Sweden amesema harusi yake ilipangwa kufanyika 21 July mwaka huu lakini Klabu yake mpya ya Malmo nchini Sweden ilimtaka afike mapema sababu utambulisho wake rasmi ulitakiwa kufanyika siku iliyofuata baada ya harusi yake, hivyo ilibidi achangamkia dili hilo jipya la kazi na kuomba ndugu yake wa kiume amuwakilishe katika harusi yake na ikawa hivyo
Hata hivyo, hadi sasa Bado hajakutana tena na mke wake ila amesema muda sio mrefu watakutana ili waende fungate(honeymoon) pamoja, amesema washinde ligi moja kwanza ndie akutane na mke wake wafurahie ndoa yao mpya honeymoon
Picha zinazoonekana ni Mohamed Turay mwenyewe na mke wake hiyo sababu kabla hajaondoka kwenda Sweden walifanya pre-wedding photo shoot na alizipost
Kabla ya kusainiwa na klabu hiyo ya Sweden, Mohamed alichezea klabu ya nchini China kwa misimu miwili