MJANE Doreen Apokea Watoto 3 wa Mrema wa nje ya ndoa



MJANE wa Marehemu Agustino Mrema amesema hadi sasa ameshapokea watoto watatu wa nje ya ndoa wa mume wake ambao walikuwa hawajapokewa na kwamba kitendo hicho ni kutimiza husia wake kwake kabla ya kufariki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Doreen ameyasema hayo leo Jumanne tarehe 30, Agosti, 2022, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi ikiwa ni siku chache tangu kuzikwa kwa Mrema.

“Kabla hajafariki Baba (Mrema) alinihusia niwapokee na kuwalea kwa upendo na umoja watoto wake wote waliopo na hata wale watakaoibuka baadae na kusema ni wanae, akanielekeza nisiogope, niwapokee, nimuombee radhi kwenu, niwakumbatie na kuwalea kama ambavyo angefanya yeye,” amesema Doreen na kuongeza;

“Mpaka sasa nimeshawapokea watoto watatu (3) ambao walikuwa bado hawajapokelewa na nilishaambiwa hivyo na Mzee Mrema siku mbili kabla ya kifo chake.”


Aidha amesema muda sahihi ukifika nitasema ukweli wote ikwemo masuala ambayo yameibuliwa na vyombo vya habari.

“Muda ukifika nitasema, siogopi na Mzee Mrema alisema nisiogope hata wakati akiwa hayupo,” amesisitiza.

Inadaiwa kumekuwepo na mgogoro mkubwa baina ya ndugu wa Mrema na Doreen ambao ulianza hata kabla ya maziko yake ambapo ndugu hao waliitoa matairi gari ambayo ilikuwa itumike na ndugu wa mwanamke huyo kwenda msibani Moshi.


Inaelezwa kuwa gari hiyo aina ya Toyota Harrier ilitolewa matairi yote manne ikiwa nyumbani kwa Mrema Salasala jijini Dar es Salaam ikiwa tayari imeshapakiwa mizigo ya ndugu wa Doreen, kitendo ambacho kilionesha ndugu hao kumtenga.

Taarifa zaidi kutoka ndani ya familia hiyo zinaeleza kuwa matairi hayo yalitolewa na mkwe wa Mrema ambaye inadaiwa alieleza kufanya hivyo kwasababu hawamtambui Doreen kama sehemu ya familia hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad