MKE wa marehemu Augustine Mrema, mwanasisasa mashuhuri nchini aliyefariki dunia 21 Agosti na kuzikwa juzi Alahmisi, Doreen Kimbi Mrema, ameanza kuonja joto ya jiwe kutoka kwa familia ya kiongozi huyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa zinasema, mjane huyo ameanza kutengwa na familia ya marehemu, wakilenga kumzuia asiondoke na chochote kutoka kwa Mrema.
Doreen na Mrema, aliyekuwa mwenyekiti wa Tanzania Lebour Party (TLP), walifunga ndoa 26 Machi mwaka huu, katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Uwomboni, Jimbo Katoliki la Moshi, mkoani Kilimanjaro, wakipishana umri kwa miaka 38.
Doreen alisema umri wa mwenza wake ni namba tu, na kusisitiza kuwa hakufuata mali kwa Mrema, mwenye umri wa miaka 77, bali ni upendo wake wa dhati alionao kwake.
Mrema alifunga ndoa hiyo, baada ya kufiwa na mke wake wa kwanza, Rose Mrema.
“Vitimbi dhidi ya Doreen, vilianza mara baada ya ibada ya kuaga mwili wa marehemu. Familia ya Mrema ilizuia gari ambalo mama alitaka kulitumia kusafirishia mizigo yake na ndugu zake, kwa kuwa yeye alisafiri na ndege, pamoja na mwili wa marehemu,” ameeleza mtoa taarifa wa MwanaHALISI.
Augustine Lyatonga Mrema, alizaliwa 31 Desemba 1945, katika kijiji cha Kilaracha kilichopo katika jimbo la Moshi Vijijini, mkoani Kililimanjaro, akiwa mtoto wa pili katika familia ya watoto watano ya Lyatonga Mrema.
Alikuwa mmoja wa wanasiasa mahiri nchini. Aliwahi kuwa naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani.
Alianza kama mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambako alikitumikia chama hicho kutoka mwaka 1965 hadi Mei 1995, alipokihama na kujiunga na upinzani.
Alisomea masomo yake ya darasani mpaka shule ya kati, huko Moshi Vijijini kati ya mwaka 1955 hadi 1963. Mwaka 1964 hadi 1965, alijiunga na Chuo cha Ualimu cha Mtakatifu Patrick.
Gari lililokuwa lisafirishe mabegi na ndugu wa mke wa Mrema ikiwa imeng’olewa matairi
Baada ya kumaliza mafunzo yake ya ualimu na kupata kazi, Mrema alianza kuchukua mafunzo yake ya sekondari ambapo mwaka wa 1968 alifanya mtihani wake wa kidato cha nne, wakati huo mitihani ikitoka Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza.
Katika kipindi cha miaka 1970 hadi 1971, alijiunga kwenye mafunzo maalumu ya siasa na uongozi katika Chuo cha Kivukoni na mwaka 1980 hadi 1981, alikuwa nchini Bulgaria, ambako alifanikiwa kutunukiwa Diploma ya Sayansi ya Ustawi wa jamii na Utawala.
Baada ya hapo, Mrema alifanya kazi mbalimbali za kijamii na kichama kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Pacific mwaka 2003, ambako alitunukiwa Shahada ya Sanaa katika Sayansi ya Jamii.
Mrema alianza kazi mwaka 1966 kama mwalimu akifundisha shule mbalimbali za mkoa wa Kilimajaro, na mwaka 1972 na 1973 aliteuliwa kuwa mratibu wa elimu wa kata