POLISI mjini Kabul wamesema watu zaidi ya 21 wamefariki kutokana na mlipuko uliotokea ndani ya Msikiti Mkubwa zaidi jijini Kabul, Kati ya hao majeruhi zaidi ya 33 wameripotiwa.
Mlipuko wa Jumatano ulitokea wakati wa maombi ya jioni, Imamu wa msikiti huo anaripotiwa kuwa miongoni mwa waliofariki.
Haijulikani ni nani aliyehusika na shambulio hilo, Ni wiki moja tangu wapiganaji mashuhuri wanaojiita Islamic State (IS) kumuua kiongozi wa kidini anayeunga mkono Taliban katika mlipuko wa bomu la kujitoa mhanga, pia huko mjini Kabul.
Mashahidi wa tukio hilo walieleza kusikia mlipuko mkubwa ambao ulivunja madirisha katika majengo yaliyo karibu na mlipuko ulipotokea.
“Niliona watu wengi sana wameuawa, na hata watu wengine walitupwa nje ya madirisha ya msikiti,” mmoja wa mashahidi alisema.
Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao