Morrison aongezewa dozi, rasmi Zalan FC kucheza Dar





KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amemwongezea  programu maalumu winga wake, Bernard Morrison ili azidi kuimarika kwa ajili ya kujiandaa na michezo mbalimbali ya Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Bernard Morrison
Septemba 6, mwaka huu Yanga watacheza dhidi ya Azam FC na Septemba 11, mwaka huu watawavaa Zalan FC ya Sudan Kusini katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana, Nabi alisema hana presha na mechi hizo mbili dhidi ya Zalan kwa sababu kikosi chake kina nafasi nzuri ya kusonga mbele ukilinganisha na wapinzani wao.

Nabi alisema, wachezaji wake wana nguvu na wako tayari kwa kupambana dhidi ya wageni hao ambao wameomba kutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kama nyumbani kwao.

Aliongeza, ana imani na kikosi chake lakini ameamua kumwongezea mazoezi Morrison ili afikie kiwango anachokihitaji kabla ya kuwavaa Zalan.


"Kulingana na ubora wa kikosi changu, nimeona nimpe Morrison (Bernard) mazoezi mengine tofauti ili kuwa imara zaidi na tayari kwa asilimia zote kwa sababu nina imani kubwa ya kufanya vizuri dhidi ya Zalan FC ili nitinge hatua inayofuata," alisema Nabi.

Aliongeza presha ya benchi lake la ufundi iko kwa Morrison ambaye kwa sasa anasimamiwa mazoezi na, Healmy Gueldich ambaye amemtengenezea programu maalum winga huyo.

“Tunahitaji kuwa na mawinga walio tayari kiushindani kabla ya kuingia katika hatua ya pili ya mtoano, tatizo Morrison bado hajawa katika kiwango bora ambacho tunakitaka, ndio maana tunamjenga zaidi,” alisema Nabi.


Alisema, anatambua kama Morrison akiwa fiti kwa asilimia kubwa jinsi alivyo hatari, anaamini anaweza  kuongeza kitu kwa kushirikiana na wengine wakiwako, Fiston Mayele na Stephan Aziz Ki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad