Kanisa la Coptic na Wizara ya afya jijini Cairo nchini Misri, wameliripoti vifo vya watu 41 na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali ya moto inayodaiwa kutokea baada ya hitilafu ya umeme katika ibada ya Jumapili.
Walioshuhudia moto huo, hapo jana Agosti 14, 2022 majira ya asubuhi, wamesema watu waliokuwa wakikimbilia katika jumba la ibada la orofa mbalimbali ili kuokoa walikuwa wakikanyagana kutokana na moto kuwa eneo la mlango wa kutokea na walizidiwa na joto na moshi.
Wakopti, ndio jumuiya kubwa zaidi ya Kikristo katika Mashariki ya Kati, inayounda angalau na watu milioni 10 kati ya Wamisri milioni 103 wenye Waislamu wengi na katika kadhia hiyo, baadhi ya wazazi walikuwa amebeba watoto nje ya jengo.
Polisi nchini Misri, imesema wengi wa waliofariki ni Vijana na Watoto. Picha na The Sudney Morning Heralrd.
Ahmed Reda Baioumy, ambaye anaishi karibu na kanisa amesema moto huo ulikuwa mkubwa na ungeweza kudhibitiwa iwapo hali ya utulivu inetawala huku shuhuda mwingine, Sayed Tawfik amesema watu wengine walijirusha nje ya madirisha ili kuepuka moto na wengi wao walijeruhiwa ama kufariki.
Mkazi wa eneo hilo, Mina Masry, alisema huduma za dharura zilichelewa kufika na Magari ya kubebea wagonjwa yalichukua zaidi ya saa moja kufika huku magari ya zimamoto nayo yakichukua karibu saa moja, licha ya kituo chao kuwa umbali wa dakika tano.
Amesema, “Kama ambulensi zingekuja kwa wakati, zingeweza kuwaokoa watu.” ambapo taarifa kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma ilionyesha kuwa kukosa hewa kulisababisha vifo hivyo, kwani wengi wao hawakuwa na majeraha yanayoonekana.
Sehemu ya Jengo la Kanisa la Coptic na lililoungua na moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme jijini Cairo nchini Misri.
Wizara ya mambo ya ndani, ilisema ushahidi wa kitaalamu ulifichua kuwa moto huo ulizuka katika kitengo cha viyoyozi kwenye ghorofa ya pili ya jengo la kanisa, ambalo pia lina huduma za kijamii.
Padre Farid Fahmy, wa kanisa lingine jirani, alisema mzunguko mfupi uliosababisha moto huo, na kwamba Umeme ulikuwa umekatika na waumini hao walikuwa wakitumia jenereta, kufanya misa ya Jumapili.
Rais wa misri, Abdel Fattah El-Sisi kupitia ukurasa wake wa Facebook “amezitaka mamlaka za nchini humo kuchunguza tukio hilo huku akiwasilisha rambirambi zake na kuzipa pole familia za marehemu na kumpigia simu Papa Tawadros II, ambaye ni Mkuu wa Kanisa la Othodoksi la Coptic kumpa pole