Msanii Harmonize Ampongeza Paula Kajala Kwa Hili "Mtoto Wangu Zuuh Atajifunza Kwako Akikua"

 


Msanii Harmonize ambaye tarehe 20 mwezi huu anatarijia kufanya show nchini Burundi, amempongeza Paulah baada ya kuzindua duka lake jipya la nguo liitwalo Paulah’s Closet lililopo maeneo ya Mlimani City (siyo ndani) jijini Dar es Salaam.


Kupitia insta story yake, Boss huyo wa Konde Gang ameandika, "Pongezi sana kwako, tuliongea kuhusu hili miaka miwili iliyopita na hatimaye ndoto imekuwa kweli. Najivunia namna ulivyokuwa sasa. Binti yangu Zuuh atajifunza zaidi kutoka kwako Inshallah" - ameandika Harmonize kumpongeza @therealpaulahkajala


Mbali na Harmonize, Puala pia amepata pongezi kwa watu wengine wengi wanaoona mambo kwa mtazamo chanya, kufuatia kuweza kumiliki duka hilo akiwa na umri wa miaka 20 tu huku kukiwa na warembo kibao mjini ambao wameishia kwenye biashara zisizo rasmi katika jamii.


Itakumbukwa, Paulah’s Closet lilizinduliwa Ijumaa ya Agosti 5, 2022 na kupewa baraka zote na mama yake, @kajalafrida na pamoja na Harmonize ambao walihudhuria tukio hilo lililoitwa "Pink Friday"


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad