Usiku wa kuamkia leo August 8,2022 Jiji Dar es Salaam kumefanyika show ya #summerApplified ambapo msanii wa muziki kutokea nchini Nigeria Kizzdaniel alitegemewa kutumbuiza kwenye show hiyo lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo
Pamoja na Kizz Daniel kutua kwenye ardhi ya Tanzania staa huyo hakufanikiwa kufanya show hiyo. Sababu za Kizz Daniel kutotokea Jukwaani hazijafahamika mpaka sasa. Tunajaribu kuwasiliana na uongozi wa waandaji wa show hiyo kujua nini haswa kimepelekea staa huyo anayetamba na wimbo wake #buga kuingia Mitini
Pamoja na Kizz Daniel kutotokea jukwaani mastaa wengine kutokea nchini Tanzania kama Marioo, Saraphina, Mabantu naYounglunya walifanikiwa kutoa burudani kwenye show hiyo
Kiingilio cha Show hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa #WareHouse zamani Nextdoor kawaida ilikuwa ni shilingi 80,000 na VIP ni shilingi150,000.