Mwanamuziki wa Kike Tokea Kenya, Avril Amkana Diamond Platnumz Katu Katu


Mwanamuziki wa kike tokea Kenya, Avril bado ameendela kukanusha rumors za yeye kuwahi kutoka na Diamond huku akiweka wazi namna urafiki wao ulivyo.


Kwenye moja ya interview aliyo ifanya hivi karibuni nchini Kenya, Avril amedai Diamond ni rafiki bora kwake na huwa hawaongei ila ikitokea wamewasiliana, basi ni maongezi ya maana, kuna muda akitaka kutoa wimbo lazima amcheki Diamond, maana anayathamini sana mawazo yake na pia ana mchango mkubwa kwenye muziki wake.


Rumors za wawili hao kuwa wanadate zilianza tokea mwishoni mwa mwaka 2012, Avril alipo shiriki kwenye video ya KESHO ya kwake Diamond kama video vixen. Video hiyo imekuwa directed na Ogopa Videos tokea Kenya, na hadi sasa ina zaidi ya views milioni 3 YouTube.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad