Mwanariadha wa Tanzania atolewa mashindao ya madola



MWANARIADHA wa Tanzania wa  mbio fupi  kwa wanawake, Winfrida Makenji ameondolewa kushiriki mashindano  ya mbio fupi yanayoendelea jijini Birmingham, Uingereza.

 Winfrida ameondolewa kwenye michuano hiyo leo Agosti 2, 2022 baada ya kukutwa na kosa katika kuanza mbio za mita 100 katika Uwanja wa michezo wa Alexander jijini Birmingham, Uingereza.

Katika taarifa ya Kocha wa Raidha, Suleiman Nyambui iliyotumwa kwenye vyombo vya Habari, inasema kuwa hofu, kukosa uzoefu vimechangiwa kwa mchezaji huyo kuondolewa mashindanoni.

 “Winfrida ni  mkimbiaji hodari ila hofu ya mashindano pamoja na kukosa uzoefu wa kushindana mara kwa mara vimechangia kuondolewa kwake mwanzo tu wa kuanza mbio.” Amesema Nyambui


 
Amesema Winfrida alifanya kosa la kuchomoka kabla ya mlio wa bastola ya kuanzia kulia, ambapo katika mashindano makubwa kama hayo adhabu yake ni kutolewa (disqualified).

Hata hivyo, Nyambui amesema kuwa Winfrida bado ana nafasi ya kushiriki mchuano wa mbio za mita 200 ambao atashindana siku ya Alhamisi Agosti 4, 2022, ambapo atakimbia raundi ya kwanza. Akipita ataingia raundi ya pili siku ya pili Agosti 5.

Aidha, Nyambui amesema kesho kutwa Alhamisi Agosti 4 mwanariadha Andrew Boniface Rhobi ataingia uwanjani kuchuana  katika mbio za mita 1,500.


Rhobi, ambaye ana umri wa miaka 32  atajiunga na wanariadha wengine wa nchi mbalimbali kujaribu kuvunja rekodi ya mbio hizo za mita 1500 inayoshikiliwa na Mtanzania mwingine Filbert Bayi kwa miaka

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad