Mwimbaji wa Muziki Toka Nigeria, Kizz Daniel Ameomba Radhi Watanzania kwa Kutokutokea Kwenye Show ya Summer Amplified..Kufanya Show Bure


Mwimbaji wa muziki toka Nigeria, Kizz Daniel ameomba radhi Watanzania kwa kutokutokea kwenye show ya Summer Amplified mwishoni mwa wikiendi iliyopita na kusema haondoki Tanzania hadi afanye show Ijumaa hii Jijini Dar es salaam ambapo waliolipia awali watapata nafasi ya kutazama show bila kulipia.


"Naipenda kazi yangu, nilikuja kutumbuiza na ninakusudia kutumbuiza. Ni matumaini yangu kwamba mtanipa nafasi nyingine ya kutumbuiza Ijumaa hii." - Ameeleza Kizz Daniel akizungumza na waandishi wa habari usiku huu.


Hitmaker huyo wa "BUGA" amebainisha kwamba alikubaliana na waandaaji wa Summer Amplified kwamba ataomba radhi kwa mashabiki na kuandaa show nyingine.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad