Mwizi wa mbwa wa Lady Gaga jela miaka minne



Mahakama ya California jana (Jumatano) imemuhukumu kifungo cha miaka minne mtu mmoja kati ya watatu walioshtakiwa kwa kupora mbwa aina ya Kifaransa wa mwanamuziki maarufu duniani, Lady Gaga.
Jaylin Keyshawn White alikiri kuwa sehemu ya genge lililompiga risasi Ryan Fischer wakati akiwafanyisha mazoezi mbwa watatu mjini Hollywood Februari mwaka 2021.
Katika usikilizaji wa kesi hiyo jijini Los Angeles jana, White, ambaye sasa ana umri wa miaka 20, alikiri kufanya unyang'anyi huo na akapewa kifungo cha miaka mine jela.
Kamera za ulinzi katika eneo hilo la shambulizi zinaonyesha gari ikisimama karibu na Fischer na watu wawili wakirukia nje.
Mtu mmoja anamtaka Fischer "asalimu amri" kabla ya mapambano ambayo baadaye risasi ilisikika, na mtunza mbwa huyo anaanguka akipiga kelele.
Kila mmoja katika washambulizi hao anachukua mbwa mmoja -- Koji na Gustav -- na kumuacha Fischer akipiga kelele za kuomba msaada.
Mbwa wa tatu -- Miss Asia -- anamkibilia mtunza mbwa huyo baada ya majambazi hao kutoweka.
Unyang'anyi huo ulisababisha mwimbaji huyo wa kibao cha "Poker Face" kutoa dau la dola 500,000 za Kimarekani (sawa na zaidi ya Sh 120 milioni za Kitanzania) kwa mtu ambaye angefanikisha kupatikana kwa mbwa hao, ambao kumekuwa na ongezeko la kuwatafuta kutokana na thamani yao.
White alishtakiwa Aprili mwaka 2021 pamoja na James Howard Jackson, ambaye sasa ana miaka 19, na Lafayette Shon Whaley, ambaye ana miaka 28.
Mwanamke aliyerejesha mbwa hao kutokana na unono wa dau hilo, ameshtakiwa kwa kupokea vitu vilivyoibwa.
Mtu aliyekuwa ameshika bunduki, Jackson, aliachiwa huru kimakosa mapema mwaka huu baada ya kile polisi walichokielezea kuwa ni makosa ya kiofisi.
Wametoa dau la dola 5,000 (sawa na zaidi ya Sh12 milioni) kwa mtu atakayetoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa Jackson, wakisema anatakiwa achukuliwe kuwa ni (mwenye silaha na hatari".
Fischer alipata jeraha kifuani katika shambulio hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad