Nabi Apewa Mchongo CAF, Sasa Yanga Washindwe Wenyewe Dhidi ya Al Hilal ya Sudan




KUELEKEA katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Msaidizi wa AS Vita ya Rwanda, Raul Shungu, amempa ushauri Kocha Mkuu wa Yanga, kuwa anatakiwa kuongeza nguvu kwenye maandalizi kama anataka kufanya vizuri kimataifa, maana Ligi ya Mabingwa Afrika si lelemama.

 

Yanga imekuwa ikishindwa kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa kwa miaka ya hivi karibuni, na msimu uliopita ilikanyaga mguu tu ikatolewa katika hatua ya mwanzo kabisa.

 

Msimu huu Yanga wamepania kufanya kweli katika michuano hiyo, wakitaka kufika hadi hatua ya nusu fainali.


Kikosi cha timu ya Yanga.

Kuna dalili zote za Yanga kukutana na Al Hilal ya Sudan inayofundishwa na Frolent Ibenge, kama ikikivuka kigingi cha Zalan FC ya Sudan Kusini.

 

Shungu ametoa kauli hiyo kutokana na Yanga kuanzia hatua ya awali ambapo itacheza dhidi ya Zalan wakati Ali Hilal ikitarajia kucheza na St. George ya Ethiopia kabla ya washindi wa mechi hizo kukutana.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Shungu alisema kuwa licha ya Yanga kuwa na wachezaji wengi kutoka DR Congo lakini bado wanatakiwa kufanya kazi ya ziada ikiwa watakutana na Al Hilal ya Sudan kutokana na kocha wake kuwajua vizuri wachezaji hao.

 

“Sioni sehemu ambayo Yanga au Al Hilal zikishindwa kufanya vizuri katika mechi zao za kwanza kwa sababu msimu uliopita Ibenge ameshinda ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na RS Berkane na amefanya usajili mzuri sawa na Yanga, naona nafasi ya wao kukutana ni kubwa.

 

“Nadhani utakuwa mchezo mgumu sana licha ya Yanga kuwa na wachezaji wengi ambao ni wazoefu lakini tayari washafanya kazi na Ibenge hapa AS Vita, maana bado itawalazimu kufanya maandalizi makubwa ili kuweza kufikia malengo kwa sababu Ibenge anawajua wachezaji na ni rahisi kuweza kubadilika,” alisema Shungu.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad