Navy Kenzo Wafunguka VIDEO ya Wimbo Wao wa Manzese Ilifanywa Mara Tatu na Directors Tofauti Watatu..


 Je wajua kuwa wimbo wa "Manzese" kutoka kwa Navy Kenzo, kabla ya video rasmi kutoka, ilishafanywa mara tatu na directors watatu tofauti?


Hilo limethibitishwa na @navykenzoofficial wenyewe baada ya kumrushia shabiki mmoja picha za ushahidi baada ya kudai kwamba wanapigwa na story ya kuwepo video mbili za "Manzese" kabla ya hii tunayioona.


SnS tumeelezwa kwamba, baada ya audio ya wimbo "Manzese" kukamilika, Navy Kenzo walimuita Director wao ambaye hufanya nae kazi mara nyingi, Justin Campos lakini alishindwa kuja kwa sababu kipindi hicho Uingereza ilikuwa katika Lock Down ya kirusi cha Omicron ndipo wakaamua kumuita Director mwingine kutoka South Africa.


Na katika kufanywa kwa video hiyo, msanii @madeeali alihusu kwenye chupa hilo, baada ya video hiyo kukamilika. Hata hivyo Navy Kenzo walipewa video ambayo haikuwa kama vile wao walivyotaka na kutegemea. Hivyo wakaona sio kweli na kumuita Director mzawa kutoka hapa nchini kushoot upya lakini tena video walipopelekewa haikuwa katika ukubwa ambao wao waliitaka. SnS tumeelezwa na chanzo cha kuaminika.


Aidha, na muda huo Director wao waliezoea kufanya nae kazi mara nyingi, Justin Campos alikuwa kasharudi South Africa, ndipo Navy Kenzo wakakwea pipa na kwenda kwa Madiba kushoot chupa lingine ambalo ndio tunaliona sasa likiwa limebeba kwa ukubwa wimbo huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad