Ng'ombe wanaofugwa kwa stress wana nyama ngumu



 
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila amewataka wadau wa mifugo kutoa elimu ya ufugaji bora kwa wafugaji ili kuwawezesha kufanya ufugaji wa kisasa ambao utaepusha ng'ombe kutembea umbali mrefu kutafuta malisho na kusababisha nyama yake kuwa ngumu
Amesema hali hiyo huchangia wafugaji kuendelea kuwa maskini kutokana na nyama kukosa soko.

Akizungumza wakati wa kufunga maonyesho ya wakulima - Nanenane - Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa ili kuhakikisha inapatikana nyama laini na yenye soko lazima elimu itolewe kwa jamii kuanzia ngazi za chini hadi za juu.

"Jamii iache kufunga ng'ombe kwa stress, ng'ombe anatembea kutoka pori la Karagwe hadi Ngara, kesho wamchinje lazima nyama yake iwe ngumu" amesema Chalamila.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad