Ni Kweli Putin Hawezi Kufa?, Nadharia Pamoja na Wasomi Mbalimbali Wametoa Ushuhuda

 


KAMA unapenda kusoma makala na kusikiliza documentary kwenye YouTube, basi utakuwa umekutana na makala na documentary nyingi zinazodai kuwa, eti Rais wa Urusi, Vladimir Putin hawezi kufa!

 

Unawezea ukajiuliza wanaosema hivyo wana hoja au vigezo gani hasa mara baada ya nchi yake kuivamia Ukraine na kuua maelfu ya watu tangu Februari 24, 2022 hadi leo huku mwenyewe akitamba kwamba hakuna kinachoweza kumuua?


Rais Putin akiwa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis

Hoja yao imeegemea kwenye kitu kinachoitwa kitaalam Quantum Immotality.

 

Hii ni nadharia ya kukwepa kifo. Je, ni kweli Rais Putin anaishi milele?

 

Katika moja ya makala za kisayansi inaelezwa kuwa ubongo wa mwanadamu haujawahi kuwaza kitu ambacho hakipo au hakijawahi kuwezekana au kuja kuwezekana!

 

Kwenye dunia hii kuna mengi ya kujifunza kuhusu maisha na vilivyo nyuma ya maisha ya kawaida.

 

Wakati mwingine nadharia hiyo inatutaka tukubali kuwa kuna nguvu nyingine inayoendesha na kutawala dunia hii tofauti na ubidamu.

 

Wapo wanaosema wazungu wamekuwa na michezo ya kutuchezea Bongo zetu kwa namna mbalimbali na kwa mambo ambayo hatukuwahi hata kuyafikiria.


Nadharia zinadai kuwa Putin anaweza kuishi milele

Dan Brown; ni mwandishi nguli wa vitabu vya kufikirika ambaye anasema kuna ‘fictions’ nyingi mno kuhusu ishu hiyo, lakini hata kama hazipo huwa zinapenyeza ujumbe uliojificha.

 

Anasema kuwa, ni wewe na imani zako tu kwa sababu imenenwa imani huponya.

 

Rais Putin anatajwa kuwa ni kati ya watu wanaodhaniwa kuwa ni ‘immortal people’; yaani watu wasiokufa.

Cc; @sifaelpaul

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad