Nickson afikishwa Mahakamani kwa kujifanya Rais Samia




Mkazi wa Mwanza, Nickson Mfoi (20) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kujifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye mtandao.

Mshitakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate na kusomewa mashitaka mawili na Wakili wa Serikali, Ashura Mnzava.

Katika shitaka la kwanza, Mnzava alidai kuwa Spetemba 22, 2021 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa nia ya ulaghai na udanganyifu Mfoi alijiwasilisha mtandaoni kama Rais Samia Suluhu Hassan jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Alidai katika shitaka la pili mshitakiwa alikutwa akimiliki na kutumia laini ya simu iliyo katika umiliki wa mtu mwingine bila kutoa taarifa kwa mtoa huduma.


 
Katika shitaka hilo ilidaiwa Oktoba 2, 2021 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mshitakiwa huyo alikutwa akitumia laini hiyo yenye namba 0686 623299 iliyo katika umiliki wa jina la Getness Jackson bila kutoa taarifa ya mabadiliko ya umiliki kwa mtoa huduma.

Baada ya kusoma mashitaka hayo, Mnzava alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na aliomba tarehe ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 18 mwaka huu wakati kijana huyo atakaposomewa maelezo ya awali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad