Odinga kwa Miaka 25, Hatma Yabaki Mahakamani




RAILA Odinga mgombea wa kiti cha uraisi wa Azimio la Umoja amepoteza tena kwa mara ya tano dhidi ya mpinzani wake William Ruto aliyetangazwa mshindi kwa asilimia 50.49% huku Raila akivuna asilimia 48.85%.

 

Mnamo mwaka 1997 kupitia chama chake cha National Democratic Party alichokiunda baada ya kujiondoa FORD-K Raila Odinga aligombea nafasi ya kiti cha Urais na kushindwa.

 

Mwaka 2002 kupitia LDP waliungana na NAK na kuunda NARC iliyomshinda Uhuru Kenyatta lakini mwaka huu Raila Odinga hakuwania kiti cha Uraisi.


Raila Odinga

Ulipofika mwaka mwingine wa uchaguzi 2007 Raila Odinga aliingia kwenye mbio za kuwania kiti cha urais kwa mara ya pili dhidi ya Mwai Kibaki na kushindwa.

 

Mwaka 2008 aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Kenya na hii ilikuja baada ya machafuko yaliyosababishwa na wafuasi wa Raila Odinga kupinga matokeo ya uchaguzi ambayo yalisababisha vifo vya raia wa Kenya zaidi ya elfu mbili.

 

Mwaka 2013 aliingia tena kwenye kinyang’anyiro cha kiti cha urais kwa mara ya tatu kupitia chama cha CORD dhidi ya mpinzani wake Uhuru Kenyatta na kushindwa.

 

Mwaka mwingine tena wa uchaguzi mkuu nchini Kenya 2017, Raila Odinga aligombea tena nafasi ya Uraisi kwa mara ya nne kupitia chama cha NASA dhidi ya mpinzani wake Uhuru Kenyatta na alishindwa.


Rais Mteule wa Kenya William Samoei Ruto

Odinga alipinga matokeo ya uchaguzi huo mahakamani kuwa ni batili na kutaka uchaguzi urudiwe, na baadaye akatangaza kujiondoa rasmi kwenye uchaguzi.

 

Mwaka huu wa 2022 aliwania kiti cha urais kwa mara ya tano kupitia chama cha muungano wa Azimio la Umoja dhidi ya mpinzani wake Willium Ruto na Kushindwa.

 

William Ruto kupitia tiketi ya chama cha UDA ameibuka kidedea baada ya matokeo kutangazwa kama Rais mteule, hata hivyo Odinga alijitokeza hadharani kupinga matokeo hayo akiyaita ni batili na hayuko tayari kuyapokea.

Imeandikwa: Simon J. Molanga kwa msaada wa mitandao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad