Polisi Wakiri Kumuua Mwanakijiji Dodoma



By Ramadhan Hassan

Dodoma. Mkazi wa kijiji cha Chioli, kata ya Songolo wilayani Chemba, Mkoa wa Dodoma, Nada Songo (45), ameuawa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kuwashambulia askari na wananchi kwa mishale yenye sumu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 29, 2022, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amesema jana Jumapili mtuhumiwa huyo alifanya matukio hayo katika kijiji hicho.

Amesema mtuhumiwa huyo amefariki mara baada ya kupigwa risasi na askari maeneo ya kifuani na mguu wa kulia wakati akiwashambulia askari hao kwa mishale inayodhaniwa kuwa na sumu.

Amesema marehemu alikuwa anakaidi kukamatwa kuhusiana na kosa ambalo alikuwa anatuhumiwa nalo la kutishia kuwaua wananchi kwa silaha za jadi.


Amesema chanzo cha tukio hilo ni Agosti 27, 2022, mtuhumiwa alishambulia wanakijiji kwa kuwatishia kwa mishale yenye sumu.

“Askari polisi walipokwenda kwa ajili ya ukamataji, mtuhumiwa alitoroka na kukataa amri halali ya kukamatwa kuhusiana na makosa yake.

Amesema Agosti 28, 2022 polisi walipata taarifa ya kurejea kwa mtuhumiwa huyo huku akiendelea kutishia usalama wa watu katika kitongoji hicho.

Kamanda Otieno amesema askari walipokwenda kumkamata aliwashambulia kwa kutumia mishale ambayo inadhaniwa ina sumu na kumjeruhi askari namba H.9377 PC William.

Amesema askari huyo amejeruhiwa  tumboni upande wa kushoto na akari wa akiba aitwaye Madodo Juma ambaye alijeruhiwa kwa mshale mguu wa kulia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad