Polisi Wasimamishwa kwa Kumpiga Raia

  


Polisi watatu katika jimbo la Arkansas nchini Marekani, wamesimamishwa kazi kutokana na video iliyozaagaa mitandaoni ikiwaonesha wakimpiga mshukiwa mmoja huku wamemlaza chini 

Mmoja wa maofisa ameonekana akimpiga mtu huyo kichwani mara nyingi huku akimpigiza kichwa kwenye sakafu


Ofisa mwingine wa polisi ameonekana amepiga magoti  huku anampiga mshukiwa huyo  


Mtu huyo baada ya kupigwa alionekana akijikinga kichwa chake kwa mikono yake huku akijibiringisha barabarani kujilinda


Video hiyo imetazamwa na mamilioni ya watu kwenye mitandao ya kijamii na kuzua minongóno  


Mtu huyo aliyekamatwa alikua na tuhuma za kusababisha vitisho kwenye duka moja, ambapo  polisi walipigiwa simu kuja kumkamata alijihami kwa kumsukuma askari mmoja aliyeanguka chini

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad