Polisi katika eneo la kusini mwa nchi ya Nigeria, imesema imewakamata watu watatu kufuatia ugunduzi wa miili 20 iliyokaushwa na kufichwa eneo lililo karibu na mji wa Benin katika jimbo la Edo lililo na matukio ya uhalifu uliopindukia.
Miili hiyo, ilipatikana katika jengo linaloshukiwa kutumiwa kama kaburi la vodoo, huku msemaji wa Polisi katika eneo hilo, Chidi Nwabuzor akisema maiti 15 za wanaume, wanawake watatu na watoto wawili pia zimegundulika.
Bado haijawekwa wazi, juu ya muda ambao maiti hizo zilihifadhiwa katika eneo hilo, huku maswali mengi yakitawala kuhusu kukaushwa kwa watu hao na kisa halisi kilichowafanya wauaji kutekeleza azma hiyo ambayo inastaajabisha.
Jengo ambalo maiti 20 ziligunduliwa na Polisi lilikuwa umbali wa maili tatu kutoka katikati mwa Jiji la Benin. Picha: EyeEm/Alamy.
Hata hivyo, Afisa huyo na Msemaji wa Polisi amesema Polisi wenye silaha na walinzi wa eneo hilo la Benin jimboni Edo, walivamia jengo hilo lililopo nje ya mji kufuatia taarifa waliyopewa kwa siri na raia wema.
“Mahali hapo ni chumba cha kuhifadhia maiti na mwenye nyumba anajulikana sana kama mhudumu hodari wa chumba cha kuhifadhia maiti na mwana mila, nashangaa tu jinsi alivyoleta hema yake kwenye chumba chake cha kuhifadhia maiti,” amesema Nwabuzor.
Ameongeza kuwa, ” Kuna maeneo manne vya kuhifadhia maiti katika mji huu, na mwenye nyumba inadaiwa alihama kutoka Circular ya First East na kuja hapa Barabara ya Ekewan, mimi ninamfahamu na ninahisi hili ni genge linalopinga ushindani unaoongezeka katika huduma za mazishi katika eneo hili.”
Kijana Osaro Nappiar (mwenye fulana nyeupe), ambaye amewaambia Polisi kwamba aliweka maiti ya marehemu mamake kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kinachosimamiwa na Chukwu Otu ambaye amekimbia wakati yeye alipokuwa akitafuta pesa za mazishi. Picha na Gatimash.
Urusi, Ukraine zashutumiana mapigano karibu na Nyuklia
Ugunduzi wa miili hiyo umewashitua watu nchini Nigeria na wakazi wa eneo hilo wanasema wametishwa na tukio hilo huku wakijiuliza ni vipi miili hiyo iliweza kufichwa eneo jirani na wanapoishi bila majirani kufahamu.
Maiti hizo 20 zilizogunduliwa ni za wanaume 15, watatu wa kike na watoto wawili ambapo washukiwa watatu waliokamatwa Agosti 17, 2022 wamefahamika kwa majina ya Chimaobi Okoewu, Oko Samuel wote kutoka eneo la Afikpo Jimbo la Ebonyi na Gideon Sunday wa Jimbo la Akwa-Ibom.
Polisi imesema mmiliki wa jengo hilo lililo mita chache kutoka chumba cha kuhifadhia maiti, kando ya mteremko wa Asoro, barabara ya Ekehuan eneo la Uzebu katika mji wa Benin, Chukwu Otu amekimbia baada ya taarifa za tukio hilo kusambaa.