Raia wa Ghana wadaiwa kuiba Sh1.6 bilioni benki



Dar es Salaam. Raia wa Ghana, Valentine Zancheus (42) na mtanzania, Fortunatus Bundala(36) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka manne likiwemo la wizi na kuingilia mifumo wa Benki ya BancABC na kujipatia na Sh1.6 bilioni mali ya benki hiyo.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani leo Ijumaa Agosti 19, 2022 na kusomewa mashtaka yao na jopo la mawakili watatu wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga akisaidiana na Yusuph Aboud, Caroline Materu, mbele ya Hakimu Mkazi, Richard Kabate.

Wakili Materu amedai kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 48/2022 yenye mashtaka ya kula njama ya kutenda kosa, wizi, kuingilia mifumo ya kompyuta za benki ya BancABC na kutakatisha fedha kiasi cha Sh1.6 bilioni.

Washtakiwa baada ya kusomewa mashtaka hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali maalum.


Hakimu Kabate ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba Mosi, 2022 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na shtaka la kutakatisha fedha linalowakabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad