Mgombea wa urais wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga.
Akihutubia wafuasi wake katika ukumbi wa KICC mnamo Jumatatu, Agosti 22, kinara huyo wa chama cha ODM alidai kuwa rais wa Venezuela walihusika katika njama ya wizi wa kura.
Kwa mujibu wa Raila, raia hao wa kigeni waliletwa nchini kuiba ushindi wa Azimio lakini akasisitiza kuwa muungano huo una imani ya haki kupatikana.
Raila Aonya Mataifa ya Kigeni Dhidi ya Kuingilia Siasa za Kenya: "Achaneni na Sisi"
“Tuna ushahidi tosha kuonyesha kuwa raia wa kigeni, hao watu kutoka Venezuela, waliletwa nchini kujaribu kuiba ushindi watu lakini hilo halitawezekana,” Raila alisema.
Suala la raia wa Venezuela ni moja ya hoja ambazo Raila aliwasilisha katika rufaa yake kwenye Mahakama ya Upeo.
Katika kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais, mawakili wa Raila wanahoji kuwa raia hao watatu wa Venezuela walikuwa na uwezo wa kupata data za IEBC na kuzikarabati.
Julai mwaka huu, raia hao watatu wa Venezuela - Jose Gregorio Camargo Castellanos, Joel Gustavo Rodriguez Garcia na Salvador Javier Sosa Suarez walikamatwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta baada ya kupatikana na vifaa vya uchaguzi.
Katika uchunguzi uliofuata, majasusi walitaka kujua mbona vifaa vya uchaguzi vilikuwa visafirishwa na watu binafsi badala ya kuletwa nchini kwa shehena.
Baadaye IEBC ilisema kuwa watatu hao walikuwa wafanyakazi wa Smartmatic International B.V., kampuni waliokuwa nayo kwa makuliano ya kiteknolojia katika uchaguzi wa Agosti 9.
Amos Wako Athiitisha Kuhusu Utayari wa Ombi la Azimio Kupinga Ushindi wa William Ruto
Kwa mujibu wa IEBC watatu hao walishikwa bila sababu madhubuti baada ya kuwasili nchini.