Taasisi ya utafiti ya Trends Insights for Africa (Tifa), imetoa maoni ya wananchi kuhusu nani atakayeshinda kiti cha urais, ambapo mgombea urais kwa tiketi ya Azimio la Umoja, Raila Odinga ameendelea kuongoza kwa kura za maoni kwa asilimia 49, akifuatiwa na mpinzani wake William Ruto mwenye asilimia 41.
George Wajackoya wa chama cha Roots, yeye ana asilimia 1.9, na David Mweure wa Chama cha Agano akiwa na asilimia 0.2, ambapo asilimia 8 hawajaamua nani watampigia kura.
Leo ndiyo siku ya mwisho kisheria, kwa kwa makampuni ya utafiti kutoa matokeo ya kura za maoni huku Raila Odinga akiongoza kwa asilimia nyingi zaidi, ambapo muafaka wa matokeo utafikiwa Agost 9 mwaka huu katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.