Rais Samia Ateua Viongozi Wawili



Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua, Eric Hamissi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL).


Kabla ya uteuzi huo, Hamissi alikuwa nje ya uteuzi baada ya kutenguliwa katika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Julai 4, 2022.


Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imesema uteuzi huo unaanza leo Alhamisi, Agosti 4, 2022.


Mbali na Hamisi mwingine aliyeteuliwa ni Stephen Kagaigai kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).


"Kagaigai anachukua nafasi ya Balozi Herbert Mrango ambaye amemaliza kipindi chake," imeeleza taarifa hiyo.


Kabla ya uteuzi huo, Kagaigai alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, kabla ya kuachwa Julai 28, 2022, katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa.


Aidha, Kagaigai amewahi kuwa Katibu wa Bunge la Tanzania

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad