Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu Mhe. Abdallah Ulega, akiwa kwenye ziara yake Wilaya ya Buchosa, Mwanza amesema Serikali mwaka huu itawakapesha wavuvi nchini kote boti za kisasa zaidi ya 150 ili wavuvi waweze kuboresha shughuli zao na kuongeza uzalishaji wa samaki.
Waziri Ulega amesema kwenye boti hizo zitafungamanishwa na teknolojia za kisasa zitakazomsaidia mvuvi kurahisisha shughuli za uvuvi.
.
Waziri Ulega aliendelea kufafanua kuwa Mhe. Rais Samia anataka kuwatoa wavuvi katika uvuvi wa kuwinda na kufanya ufugaji wa kisasa wa uhakika.