Rais wa FIFA na Rais wa CAF Kushuhudia Mchezo wa Yanga na Simba Leo



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa amewaomba Rais wa Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’ Gianni Infantino na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ Patrice Motsepe kuwa sehemu ya watakaoshuhudia mchezo wa Kuwania Ngao ya Jamii, Jumamosi (Agosti 13), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mabingwa wa Tanzania Bara Young Africans watacheza dhidi ya Simba SC katika mchezo huo, ambao utatumika kama kiashirio cha kufunguliwa kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/23.

Waziri Mkuu Majaliwa amewaomba viongozi hao, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 44 wa kawaida wa ‘CAF’ katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa ‘AICC’ jijini Arusha mapema leo Jumatano (Agosti 10), ambapo Tanzania imebahatika kuwa mwenyeji kwa mara ya kwanza.

Waziri Mkuu pia amewaomba Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ‘CAF’ kufika Dar es salaam kutazama mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini Tanzania.

“Simba, Young Africans na Azam FC ni vielelezo vya soka la Tanzania. Naomba tarehe 13 mje uwanja wa Mkapa kutazama Derby ya Kariakoo ambapo ni Derby kubwa na yenye mvuto barani Afrika” amesema Waziri Mkuu Majaliwa

Msimu uliopita Simba SC ilipoteza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Young Africans kwa kufungwa 1-0, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, bao likifungwa na Mshambuliaji kutoka DR Congo Fiston Mayele.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad